WELCOME ALL

Gonga Hapa.

Wednesday, April 6, 2011

UKEKETAJI BARANI AFRICA




Mara nyingi tendo la ukeketaji unaitwa pia "tohara" kwa kulifananisha na upasuaji mdogo wa wanaume, lakini mambo ni tofauti kabisa.


Hapa sehemu za nje za viungo vya uzazi zinakatwa kusudi wasifurahie sana tendo la ndoa, hivyo wawe waaminifu zaidi kwa waume wao.

Ukeketaji umeenea hasa kati ya mataifa na makabila wenye asili ya bonde la Naili na majirani wao.

Kinyume na tohara ya wavulana matabibu wanaona hasara nyingi katika desturi hiyo. Ukeketaji unasababisha wasichana wengi kufa na wengine wengi kupatwa na maumivu makali wakati wa hedhi, wa tendo la ndoa na wa kujifungua.

Kwa sababu hizo serikali nyingi za dunia zimeupiga marufuku.

Pia madhehebu kadhaa yanatoa mafundisho kuwa ni kinyume cha masharti ya dini yao.

Mkeketaji kwa lugha ya kiswahili huiitwa “Ngariba”



Madhara ya ukeketaji
Kuhusu madhara kwa wanaokeketwa yapo mengi kwa na kuwa yamekwishatokea na kuwa malalamiko yapo mengi miongoni mwa waathirika.

“Unaweza ukakosa hamu ya kufanya ngono, au ukajifungua kwa tabu, kwa kweli madhara yapo mengi.
"na vile vile huweza kusababisha maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi kwani vifaa vinavyotumika hurudiwa kwa wasichana wengi hivyo kuweza kusababisha usambazaji wa VVU.

UUAMBUKIZO huu unaleta maumivu makali na kutoa maji maji yenye madhara makubwa, kwa sababu maji maji hayo huweza kusambaa na kuweza kuingia kwenye mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi na hata kwenye mayai na kusababisha kuwepo kwa tatizo lisilokwisha.

Wanawake wengine huishia kuwa wagumba kwa sababu baadhi ya viungo vyao vya uzazi huharibiwa moja kwa moja, kiasi cha kutoweza kufanyiwa marekebisho tena

Wakati wa kupona baadhi ya wanawake hupata kovu lenye kitundu (keloid) na kufanya njia au uzazi kuwa ndogo.

Wapo wanawake kutokana na kukeketwa, hushindwa kushiriki vizuri tendo la ndoa kutokana na kupata maumivu na kukosa hisia, kufuatia kukatwa kwa kisimi ambacho ni sehemu muhimu kwa wanawake ili kufurahia tendo hilo.

Kwa wale wanaokeketwa au kushonwa, hali inakuwa mbaya zaidi kwa sababu mwanaume anaweza kushindwa kushiriki, kwani njia ya uke ni ndogo, hali hiyo inasababisha baadhi ya wanawake kukatwa tena ili kupanua njia.

Wanawake waliokeketwa, baadhi yao hupata shida wakati wanakwenda hedhi kwa vile njia ya uke huwa ni ndogo, hali hiyo husababisha mwanamke mwenye tatizo hili kuvimba tumbo kwa kuwa damu hushindwa kutoka nje na badala yake hujaa tumboni.

Hali hii kwa wasichana huweza kufanya wasiweze kuona damu ya hedhi na hivyo huweza kuhisiwa kuwa wana mimba na hivyo kumletea madhara.


Matatizo wakati wa ujauzito na wakati wa kujifungua hutokea mara nyingi kwa wanawake waliofanyiwa ukeketaji.


Iwapo mimba itaharibika, mabaki ya kitoto yanaweza kubaki kwenye mfuko wa uzazi na njia ya uzazi, kuwapo kovu kusababisha nyama zilizopo kwenye njia ya uzazi kushindwa kunyumbuka na kwa hali hiyo mama mjamzito kushindwa kujifungua.

Hali hiyo ya kushinda kujifungua, huweza kusababisha kifo kwa mama na mtoto aliyeko tumboni.

Mama anayejifungua anaweza kuchanika msamba ambapo sehemu ya uke na haja kubwa huungana. Uchanikaji huo humfanya mwanamke anayejifungua kupoteza damu nyingi.

Kwa kuchelewa kujifungua, mtoto anaweza kuharibika ubongo au kufa. Ili kuzuia hali hiyo isitokee, mama aliyekeketwa na kushonwa, atatakiwa kuchanwa upya ili mtoto aweze kupita bila ya matatizo.

Hata hivyo, iwapo mama huyo atajifungua nyumbani na hivyo kukosa mtu wa kumkata sehemu hiyo aliyoshonwa, atachelewa kujifungua. Basi hali kama hii itakapotokea, husababisha mama kupoteza damu nyingi, kuumia sehemu zinazozunguka eneo hilo, kupasuka msamba au uambukizo.


hivi ni baadhi ya vifaa vianvyotumika kwenye tendo la ukeketaji.
kwa kuangalia kwa macho tu utahisi kama ni vitu ambavyo havina maana machoni mwako,la hasha!!!,... Mangariba hutumia vitu kama hivyo pindi wanapoanza zoezi la ukeketaji.


ni maumizi makali wanayo pata wasichana pindi wanapokeketwa kwani hakuna hapo hakuna ganzi wala dawa ya kutuliza maumivu,hakika huu ni ukatili wa hali ya juu kwa ndugu zetu wa kiafrica kwa baadhi ya makabila.

Kwa hali hiyo juhudi za harka zinahitajika katika kuelimisha jamii juu ya suala la ukeketaji,elimu itolewe ili jamii ipate ufahamu wa mila ambazo hazina msingi na zimeshapitwa na wakati kwani ni hatari sana katika maisha ya jamii inatozunguka.
BAADHI  YA MAKABILA YANAYOFANYA UKEKETAJI
Arusha, Dodoma, Mara na Kilimanjaro na Singida, umenukuu sababu kadhaa zilizotolea kuhalalisha ukeketaji wa wanawake
Sababu hizo ni pamoja na kutunza ubikira kabla ya ndoa, kupunguza hamu ya kutaka kujamiiana na kuondoa nafasi ya kuwa na uhusiano wa mapenzi nje ya ndoa halali au mwenza kujitunza na kuondoa uwezekano wa kupata maambukizi ya ugonjwa yanayosababisha na uchafu unaojulikana kama lawalawa, kuwaongezea wanawake starehe ya tendo la ngono wakati wa kujamiiana kutokana na kutokuwapo kinembe na maji maji ukeni.

Kina mama wa makamo kiumri katika vijiji vya mikoa mitano uliofanywa utafiti huu, walisema kwamba kukeketa wanawake ni ishara ya kuonyesha kuwa msichana ametoka katika kundi la utoto na ameingia katika kundi la watu wazima, mwanamke yupo tayari kukabili ndoa.

Ni mila na desturi, sherehe za wasichana kutoka katika kundi la utoto na kujiunga na wanawake, unyago hufanywa katika jamii zisizokeketa kama vile wenyeji wa Dar-es-salaam na Pwani, kabila la Wazaramo, Wamanyema Kigoma na Wamakonde wa Mtwara

"Tujiunge kwa pamoja katika kukomesha hali hii ili kuondoa mila potofu zilizopitwa na wakati: