WELCOME ALL

Gonga Hapa.

Tuesday, September 7, 2010

Ujue Mkoa wa Lindi Japo kwa Ufupi



Mkoa una wilaya sita za Lindi Mjini na Lindi Vijijini, Kilwa, Nachingwea, Liwale na Ruangwa.

Mito mikubwa ndiyo Lukuledi, Matando na Mavuji, yote yaelekea Bahari Hindi. Mwinuko huanza mwambaoni ukipanda hadi mita 500, hakuna milima mirefu sana.

Wakazi

Mwaka 2002 idadi ya wakazi ilikuwa 791,306. Karibu asilimia 90 kati hao ndio wakulima. Makabila makubwa zaidi ni hasa Wamwera ambao wanapatikana hasa wilaya ya nachingwea na lindi vijijini katika kata za Rondo halafu Wamachinga ,Wamalaba ambao wako zaidi lindi mjini Wamatumbi na Wangindo huko Kilwa.

Idadi ya wakazi wa wilaya ni (idadi katika mabano): Kilwa (171,850), Lindi Mjini (41,549), Lindi Vijijini (215,764), Liwale (75,546), Nachingwea (162,081), Ruangwa (124,516),

Hali ya hewa

Hali ya hewa ya Lindi ni ya joto mwaka wote ikiwa na wastani kati ya sentigredi 24,5 na 27. Mkoa hupokea kati ya 980 mm na 1200 mm za mvua kwa mwaka, hasa kati ya miezi ya Novemba na Mei.

Miundombinu ya Mawasiliano

Kuna barabara chache katika hali nzuri. Ndizo 155 km za barabara ya lami na 3567 km barabara za udongo, mara nyingi katika hali mbaya. Wakati wa mvua mara kwa mara njia ya kwenda Daressalaam imefungwa. Kuna matumaini ya kuboreka kwa mawasiliano na mji mkuu wa Daresalaam tangu kumalizika kwa daraja la Rufiji. kwa sasa barabara ya kutoka mingoyo mpaka dar-es salaam imekamilika kwa kiwango cha lami ni kimebaki kipande cha kilometa 60 tu kuanzia Muhoro wilaya ya kilwa mpaka kukaribia daraja la Mkapa mto Rufiji ambacho kinamaliziwa kwa kiwango cha lami

Pana kiwanja cha ndege Lindi, Nachingwea na Kilwa Masoko. Lindi na Kilwa Masoko kuna pia bandari. Huduma za simu zipata maendeleo kiasi tangu kuanzishwa kwa simu za mkononi.

Utalii haujafikia umuhimu sana kutokana na matatizo ya mawasiliano magumu ingawa Lindi ina sehemu mbalimbali zenye uwezo wa kuwavuta watalii: Kilwa Kisiwani ndicho mji wa kihistoria wa pwani la Afrika ya Mashariki pamoja na magofu ya miji mingine ya Waswahili, Selous ni hifadhi kubwa kabisa katika Afrika, ufukoni wa mchanga ni wa kuvutia sana, nafasi za zamia majini ni tele.

Gesi imepatikana baharini karibu na kisiwa cha Songosongo imeleta matumaini ya maendeleo.

Kilimo na Biashara

Mkoa wa lindi wakazi wake wengi ni wakulima hasa maeneo ya vijijini wengi wanalima mazao mchanganyiko yaani ya biashara na chakula mazao ya biashara hasa ni Korosho ambazo zinapatika kwa wingi katika wilaya ya Ruangwa,Lindi Vijijini,na Nachingwea ,pia kuna zao la Ufuta na ndizi kama zao la biashara na chakula pia Mazao ya chakula kuna mahindi,mpunga,muhogo,nyanya,vitunguu hizi pia ulimwa sana wakati wa masika kutegemea na mvua za vuli. Biashara wakazi wengi wa mkoa walindi wanafanya biashara hasa biashara ndogondogo zijulikanaza kama machinga trade wanauza mazao wakati wa mavuno na uchukua bidhaa nyingi kutoka Dar-es-salaam na kupeleka vijijini hasa kwenye kata.

Elimu

mkoa wa lindi huko nyuma kielimu kwani idadi ya shule za sekondari mpaka sasa si nyingi sana na shule hizo azina walimu wa kutosha kutokana na miundombinu ya barabara na shule zenge kidato cha tano na sita mpaka sasa ni lindi sekondari-lindi,mahiwa na namupa seminari-lindi vijijini, pia kuna chuo cha uwalimu nachingwea katika wilaya ya nachingwea






WELCOME TO KUNAMBI BLOG!!!

No comments: